Tuesday, 28 March 2017

Jokes za Uchumba

Msichana mmoja alimpeleka mchumba wake kwao kumtambulisha kwa wazazi wake.
Alipofika tu baba yake akagundua dosari maana mvulana alikuwa mweusi tii ana matege makali na makengeza ya maana!!
Jamaa alipo ona sura ya baba mkwe wake imebadilika ikabidi atabasamu kiasi.
Lahaula! Alikuwa na mapengo hana meno yote ya mbele!
Baba akaamua amuite binti yake:
Baba:”Mwanangu hebu twende nje tuongee.”
Binti:”Baba sema hapahapa tu mchumba wangu ni kiziwi.”
.
.
Baba mtu akazimia!!

Wanawake ni nomaa


 

wanawake watanunua mapochi
ya million mbili ili tu
kuringishiana wenyewe
kwa wenyewe kwa sababu 
sijawahi kusikia jamaa anasema ,

"Machizi yule demu ni mbayaaaa ila pochi lakeee ni noumaaaa"

Mchwa na nyoka

Mchwa kaingia kwa uchi wa mwanamke akidhani ni pango. Alipotoka, wenzake wakamuuliza alikokuwa tangu jana. Akasema’LOL! Jana karibu nimalizwe, ‘nimeingia pangoni..ghafla nyoka naye akaingia akitaka kuniuma. Akatia kichwa akitoa, akatia akitoa mara nyingi lakini hakunipata. Mwishowe akachoka akanitemea mate kisha akaenda zake’.

WATU NI WALEVI

                 Kuna watu ni walevi kiasi kwamba wakiona mkate wanapata hasira.

                     "HIYO NGANO SI INGETUMIKA KWENYE BIA AISEE"

Which Airline Does She Work For?

A Man Finds A Beautiful & Hot Girl In An Airline Uniform At An Airport Cafe Sitting Next To Him.
He Thinks To Himself ”She Must Be A Flight Attendant, But Which Airline Does She Work For ?
Hoping To Get Her Attention He Just Started To Say The Slogans Of Airlines
He Leans Towards Her And Says The Jet Airways Slogan ”The Joy Of Flying”
That Girl Doesn’t Pay Any Attention.
Again He Leans And Says The Kingfisher’s Slogan ”Fly The Good Times” And Again Gets No Response.
Now He Say Emirates Slogan ”Keep Discovering”
But This Time He Leans Over To Say Another Airlines Slogan. Before He Could, Girl Turns And Says: “Kya Takleef Hai Re Tere Ko Haramkhor?
Man Leans Back, Smiles And Says: “Ahhh…. Air India.

Girls are Girls After All

A Boy Is Trying To Persuade His Girlfriend.
Boyfriend: “Baby, Are You Jealous?”
Girlfriend: “Nope.”
Boyfriend: “Are You Sure You Are Not Jealous?”
Girlfriend: “No! Not At All.”
Boyfriend: “So, You Are Not Jealous?”
Girlfriend: “I Already Told You, No.”
Boyfriend: “That Is So Sweet, Can I Get A Kiss?
Girlfriend: “Go Get A Kiss From That Ugly Sick Chic Who Liked Your Pictures On Facebook.

Tust In GOD ,Always

There Was A Flood In A Village.
One Man Said To Everyone: “I’ll Stay! God Will Save Me!
The Flood Got Higher And A Boat Came And The Man In It Said: “Come On Mate, Get In!
No, God Will Save Me!” Replied The Man.
The Flood Got Very High Now And The Man Had To Stand On The Roof Of His House.
A Helicopter Soon Came And The Man Offered Him Help.
No, God Will Save Me!” He Said
Eventually He Died By Drowning.
He Got By The Gates Of Heaven And He Said To God: “Why Didn’t You Save Me?
God Replied: “For Goodness Sake! I Sent A Boat And A Helicopter. What More Do You Want!

Remi: "Carlos the Jackal" afungwe maisha

Mwendesha mashitaka nchini Ufaransa Remi Crosson du Cormier ametaka Ilich Ramirez Sanchez anayejulikana kwa jina maarufu la Carlos the Jackal ahukumiwe kifungo cha maisha jela kwa shambulizi la guruneti 1974 mjini Paris lililowazua watu wawili. 

Kesi hiyo inatarajiwa kukamilika leo na hukumu kutolewa ingawa majaji watachukua muda zaidi kuizingatai hukumu hiyo. Wakili wa Carlos,
 Isabelle Coutant Peyre amesema kesi dhidi ya raia huyo wa Venezuela mwenye umri wa miaka 67 ni ya kisiasa. 

Carlos anatumikia vifungo viwili vya maisha kwa kuhusika na mashambulizi ya mabomu yaliyowaua watu 11 kati ya 1982-83 na kwa mauaji ya mawakili wawili wa polisi ya Ufaransa na afisa wa ujasusi wa Lebanon 1975.

Amnesty: Mashambulizi ya Mosul ni kinyume na sheria

     Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema mamia ya raia wameuawa katika mji wa Mosul nchini Iraq katika miezi ya hivi karibuni baada ya maafisa kuwaamuru wabakie majumbani mwao licha ya mashambulizi ya kutokea angani ya muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu mjini humo.

 Raia hadi 150 waliuliwa katika shambulizi la kutokea angani Machi 17 katika kitongoji cha al-Jadida mjini Mosul.

Shirika hilo limesema agizo la maafisa wa Iraq lina maana vikosi vya muungano vilitakiwa kufahamu idadi kubwa ya raia wangekuwa wahanga wa mashambulizi yoyote ya kutokea angani. 

Shirika la Amnesty International linasema kushindwa kuyazuia mashambulizi hayo huenda kumevunja sheria za kimataifa. Maafisa wa Marekani na Iraq wanachunguza shambulizi hilo pamoja na mengine.


Mwanaharakati wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini afariki

    Mwanaharakati maarufu aliyepinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Ahmed Kathrada amefariki mapema leo akiwa na umri wa miaka 87.

 Wakfu wake umesema amekufa katika hospitali moja mjini Johannesburg baada ya kuugua kwa muda mfupi kufuatia matibabu ya kupasuliwa ubongo. 

Kathrada ni miongoni mwa watu walioshitakiwa katika kesi ya Rivonia 1964 iliyoibua hamasa kubwa kimataifa kuhusu ukatili wa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Kathrada alitumikia kifungo cha miaka 26 na miezi mitatu jela, 18 akiwa katika gereza maarufu la kisiwa cha Robben katika pwani ya mji wa Cape Town pamoja na rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela. 

Askofu mkuu wa Afrika Kusini aliyestaafu Desmond Tutu amemueleza Kathrada kuwa mtu aliyekuwa na wema na unyenyekevu na kumpongeza kama kiongozi aliyekuwa na maadili katika vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.


Nape Nnauye akabidhii ofisi kwa Waziri Mwakyembe

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamadunu na michezo, Nape Nnauye leo amekabidhi ofisi kwa Waziri Mpya wa Wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Dodoma.
Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye leo amekabidhi rasmi ofisi kwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na watendaji wakuu wa Wizara, Mhe. Mwakyembe ameahidi kuwa licha ya kukabidhiwa ofisi, anaamini kuwa Mhe. Nnauye bado ni mdau mkubwa wa sekta za Wizara na kuwa anategemea kuendelea kupata ushirikiano kutoka kwake.
Aidha Waziri Mwakyembe ameahidi kuendeleza yote mazuri yaliyo anzishwa na Nnauye katika kuimarisha ufanisi wa Wizara na kuhakikisha inakuwa ni moja ya Wizara za mifano nchini. Amesisitiza kuwa katika kipindi kifupi alichokaa Wizarani, Mhe. Nnauye alianzisha mabadiliko makubwa na watu wameanza kuifahamu vizuri Wizara.
Kwa upande wake Nnauye amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana kubwa ya kusimamia Wizara kwa kipindi cha miezi 15 huku akiwa ndio kwanza amekuwa mbunge katika awamu yake ya kwanza. Aidha Nnauye ameahidi kuendela kushirikiana na Wizara kwa ukaribu kwani ni kweli yeye ni mdau mkubwa wa sekta za wizara hii.
Heshima aliyonipa Rais ni kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini,”  Nnauye. Aidha alisisitiza kuwa, tofauti na maneno ya mitandaoni, yeye atabaki kuwa mtiifu kwa Rais, Serikali na chama chake.





Maamuzi ya Awadh Juma kuhusu maisha yake ya badae ndani ya Simba

    Awadh Juma (mbele) akipongezwa na wachezaji wenzake Mussa Mgosi (kulia) na Danny Lyanga (kushoto) baada ya kuifunga bao lililoipa Simba pointi tatu


KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Simba Awadh Juma ameibuka na kusema kuwa kwa sasa si mali ya klabu hiyo baada ya kuvunja nayo mkataba.
Awadh ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Mwadui FC ya Shinyanga awali wakati anajiunga na timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo msimu huu ilielezwa kwamba ametolewa kwa mkopo jambo ambalo sasa amelikanusha.
Awadhi Juma  amesema: “Nilikuwa nimesaini miaka miwili kuitumikia Simba lakini nimeona nikatishe mkataba wangu kwa kuwa sioni ninachofaidikia.”
“Nimesaini mkataba wa awali wa miezi sita na timu ya Mwadui, lakini mpaka msimu huu uishe ndiyo nitaanza kuitumikia kutokana na mimi kuwa huru kuichezea timu yoyote,” alisema Awadhi.

Aidha Awadhi Juma ambae wanamuita mfalme wa Mtani Jembe amlikuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Yanga kwenye game za Mtani Jembe alisema, anavutiwa sana na uchezaji wa Said Ndemla ambae kwasasa amekuwa anapata nafasi katika kikosi cha mwalimu Joseph Omog.

Monday, 27 March 2017

Jionee Treni inayopita kwenye nyumba za watu kuchukua abiria China

Leo March 27, 2017 esiryunza16.blogspot.com inakusogezea hii ambayo huko kwenye mji wa Chongqing China ambao ukitaka kusafiri huhitaji kuufuta usafiri bali usafiri unakufuata mpaka eneo la nyumbani kwako.
Mji wa Chongqing uliopo kusini-mashariki mwa China imeusogeza karibu na wakazi wake usafiri wa treni kwa reli kupita kwenye baadhi ya nyumba za kuishi watu pia kuna vituo ambavyo wakazi wa eneo hilo husubiri usafiri huo.
Mji huo pia unafahamika kama ‘Mountain City’ una wakazi wapatao 49 million, hivyo kuwafanya wasanifu majengo na maafisa wa mipango miji kubuni njia hiyo kurahisisha usafiri.


Polisi Afrika Kusini waonya juu ya teksi za wabakaji mjini Johannesburg

Mvulana wa miaka 10 alilazimishwa kulala kifudi fudi wakati mama yake akibakwa kwa muda wa saa nne katika teksi mjini Johannesburg , kwa mujibu wa ripoti kutoka Afrika kusini.
Yeye na mama yake wanadaiwa kulaghaiwa kuingia ndani ya teksi ya basi dogo kabla ya kufanyiwa maasi hayo na kuamrishwa kukabishi kadi yake ya benki pamoja na namba za siri(PIN) za kadi ya benki na wanaume watatu waliokuwa wamejihami kwa bunduki
Inadhaniwa kuwa kuwa hili lilikuwa ni shambulio la hivi karibuni la genge la majambazi.
Taarifa za kwanza za "teksi za ubakaji " zilitolewa mwaka mmoja uliopita.
kwa mujibu wa rekodi za Roodeport, mashambulio ya awali ya ubakaji yaliripotiwa mwezi Machi 2016, huku mashambulio matatu yakifanyika katika kipindi cha wiki ya mwisho ya mwezi Juni.
Matukio yote yalifanyika ndani ama karibu na kitongoji cha Soweto mjini Johannesburg.
hata hivyo haijabainika wazi ni mashambulio mangapi yaliyokwisha tokea huko katika kipindi cha miezi 12, ama ikiwa yote yalitekelezwa na genge hilo hilo.
Luteni kanali Lungelo Dlamini amesema: "Kikundi cha wanaume watatu ama wawili waliokuwa wakiendesha magari mawili tofauti ya [Toyota] Quantums, moja la rangi ya majivu na jingine la rangi nyeupe, yali wachukua wanawake wawili yakijifanya ni magari ya teksi, wakawapora kwa silaha na baadae kuwabaka."
Bwana Dlamini amesema kuwa haijabainika wazi kuwa magari hayo ya Quantum yalikuwa yana njama moja ama kila moja lilikuwa linatekeleza uhalifu huo kivyake

Hadi sasa, wanawake wawili -akiwemo mama wa mvulana huyo -wamekwisha zungumza na vyombo vya habari vya Afrika Kusini, kuelezea kilicho wasibu.
Mwanamke wa pili alikiambia kituo cha redio cha Kaya FM namna mwanamume aliyempata baada ya kushambuliwa aliwasaidia wanawake wengine wanaodhaniwa kubakwa katika eneo hilo hilo .
Amesema genge hilo limekuwa likiendesha uhalifu huo, kulingana mtandao wa habari wa -Afrika News network.
Wanawake wote wawili walichukuliwa nyakati za mchana.
Baada ya mama na mwanae kuingia ndani ya teksi, mvulana alilazimishwa kulala kifudi fudi chini kwenye sakafu ya gari hilo, huku wanaume watatu wakimbaka mama yake.
Muathiriwa huyo aliliambia shirika la habari la EyeWitness News kwamba alikuwa anaomba wakati wa tukio hilo majangili wasimuumize mwanae.
Afrika Kusini ina viwango vya juu vya visa vya ubakaji vinavyoripotiwa duniani.

Aliyemfunga mbwa wake mdomo atupwa jela miaka 5

Mwanamume mmoja raia wa Marekani ambaye alifunga mbwa wake kwenye mdomo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.
William Dodson, mwenye umri wa miaka 43, anasema alimfunga mbwa huyo mdomoni kwa sababu alibweka sana. Ililazimu mbwa huyo kufanyiwa upasuaji mara kadha baada ya kupoteza sehemu ya ulimi wake.
Siku moja baada ya hukumu hiyo kutolewa, William Dodson pia alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, kwa mashtaka tofauti ya bunduki.
Vifungo hiyo viwili vitafuatana.
Kulingana na polisi William Dodson alimnunua mbwa huyo kwa jina Caitlyn kwa dola 20.
Dodson, ambaye alikuwa huru kwa dhamana wakati huo, alimfunga mbwa huyo nje baada ya kumfunga mdomo wake mara tisa.
Lakini mbwa huo alifanikiwa kutoroka mwezi Mei mwaka 2015, na alikuwa mgonjwa sana wakati alipatikana akirandaranda barabarani.
Kamba aliyotumia kumfunga mbwa hiyo ilizuia damu kufika hadi kwenye ulimi wake, na iliwachukua madaktari wa mifugo karibu saa 36 kuiondoa.
Wakati huo chama cha wanyama cha Charleston, kibadilisha picha ya akaunti yake na kuweka picha ya mbwa huyo, kama njia ya kuonyesha uzalendo.
Wamekuwa wakichapisha taarifa jinsi mbwa huyo anavyoendelea katika kisa hicho kilichoangaziwa kimataifa.
Caitlyn, alikuwa na umri wa miezi 15 wakati alipatikana na sasa amehitimu miaka mitano akiwa anaishi na familia tofauti.

Mwanamuziki Ney wa Mitego aachiliwa huru

Mwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi Tanzania kuhusiana na wimbo wake, ameachiliwa huru.
Wa Mitego ameachiliwa huru saa chache baada ya Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe kuagiza aachiliwe huru.
"Saa hizi sina kubwa la kuongea. Wimbo umeruhusiwa. Nashukuru. Nafurahi kusikia taarifa ya serikali kwamba wameruhuru wa Wapo upigwe. Upigwe kwa nguvu," amesema Wa Mitego baada ya kuachiliwa huru.
Kuhusu kuuboresha wimbo huo, amesema: "Hili nitalifanyia kazi. Siwezi kusema saa hizi ni vitu gani kwa sababu ndio nimetoka huko. Lakini nitalifanyia kazi kwa sababu tayari ni wimbo wa kila mtu, wimbo wa Watanzania, wimbo wa watu wote."
Dkt Mwakyembe hata hivyo alimtaka Ney wa Mitego auboreshe zaidi wimbo wake, kwa mujibu wa ujumbe uliopakiwa katika ukurasa Rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kwenye Twitter.
Sehemu ya maudhui ya wimbo huo inagusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.
Mapema leo, Baraza la Sanaa la Taifa Tanzania (Basata), lilikuwa limetangaza kuufungia wimbo huo kwa jina Wapo usichezwe kwenye vyombo vya habari au kutumika kwa namna yoyote ile.
"Basata linawakumbusha wasanii na wadau wote wa kazi za sanaa kuzingatia ubunifu wa hali ya juu kufanya kazi za sanaa, hata kufikisha ujumbe mbalimbali wa kufundisha, kuelimisha, kuburudisha na hata kuonya," taarifa kutoka kwa baraza hilo ilisema.
"Baraza linawaonya wale wote wanaotumia kazi zilizopigwa marufuku, ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi (na) hatua kali zitachukuliwa juu yao."
Awali kulikuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba Rais wa Tanzania John Magufuli alikuwa ameagiza wimbo huo uendelee kuchezwa.
Kiongozi wa upinzani kutoka chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe hata hivyo alionekana kukerwa na taarifa hizo.
Bw Kabwe alisema Rais hana mamlaka yoyote ya kuamua wimbo uchezwe au usichwezwe.
"Ilikuwa ni makosa kumkamata Ney na agizo la Rais halina maana pia," aliandika kwenye Twitter.

Ripoti: Faru John alikufa kwa kukosa uangalizi wa karibu Tanzania

Faru maarufu kwa jina John, ambaye alikufa mwaka jana nchini Tanzania, alikufa akiwa katika hifadhi ya Sasakwa Grumeti kwa kukosa matunzo na uangalizi wa karibu, ripoti ya uchunguzi inasema.
Uchunguzi huo ulioongozwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele uligundua kuwa kulikuwa na mapungufu katika kumtunza mnyama huyo kabla ya kufa kwake
Prof Manyele amesema miongoni mwa mengine, hakukuwepo na kibali rasmi cha kumhamisha Faru John.
Aidha, hakukuwa na mkataba wa kupokelewa kwa Faru John hifadhi ya Sasakwa Grumeti na afya na maendeleo ya Faru John baada ya kuhamishwa haikufuatiliwa.
Prof Manyele alisema hayo alipowasilisha ripoti ya uchunguzi kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.
"Sababu za kifo chake zilichangiwa na kukosa matunzo na uangalizi wa karibu, kukosa matibabu alipoumwa, mazoea yanayotokana na kutofuata taratibu zilizowekwa kisheria na mapungufu ya kiuongozu kwa Wizara husika, hifadhi na taasisi zake," alisema.
Maabara iliyotumika ni ya Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini chini ya usimamizi wa timu ya wataalamu kutoka Tanzania, wachunguzi wa Serikali, chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Prof Manyele amesema tume yake ilifanya uchunguzi wa kifo cha Faru John kwa kupima vinasaba vya sampuli mbalimbali vikiwemo mzoga, fuvu, mifupa, pembe, damu, ngozi na kinyesi kilichokaushwa ambapo ilibainika kuwa vyote ni vya mnyama mmoja, aina ya faru mweusi ambaye ni dume.
Waziri Mkuu aliiunda tume hiyo Desemba 10, mwaka jana baada ya kupokea pembe mbili za faru John na taarifa yenye nyaraka zilizotumika kumhamisha faru huyo.
Hatua hiyo ilifuatia agizo alolitoa Desemba 6, 2016, akiwa ziarani mkoani Arusha, ambapo alitoa siku mbili na kuutaka uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru John kutoka kwenye hifadhi hiyo.
Alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Wasichana waliovalia nguo za kubana wazuiwa kusafiri na ndege ya United Airlines Marekani

Shirika la ndege la United Airlines nchini Marekani limeshutumiwa sana baada ya kudaiwa kuwazuiwa wasichana wawili waliokuwa wamevalia suruali ndefu za kubana kusafiri na  ndege hiyo.
Kisa hicho kilitokea kwenye safari ya ndege iliyokuwa ikitokea Denver kuelekea Minneapolis Jumapili asubuhi, mwanaharakati Shannon Watts amesema.
Shirika la United limesema wasichana hao walikuwa wanasafiria hati maalum, ambayo hutumiwa na wafanyakazi wa shirika la ndege na wageni wao.
United wamesema huwa kuna kanuni za mavazi kwa wanaotumia hati hiyo kusafiria.
Shirika hilo limefafanua kwamba abiria wa kawaida, ambao wanalipia tiketi zao, wako huru kuvalia mavazi yao ya kubana.
  • Hati hiyo maalum ya kusafiria ya United huwawezesha walio na hati hiyo kusafiri kwa ndege bila malipo au kwa tiketi za bei nafuu sana.
Kanuni za mavazi kwa wanaotumia hati hiyo hueleza kuwa hawafai kuvalia mavazi ya kubana, iwe ni blauzi za lycra/spandex, suruali ndefu au rinda.
Aidha, hawaruhusiwi kuvalia mavazi yanayoanika vitovu vyao au minisketi.
  • Mwanaharakati Shannon Watts ameandika kwenye Twitter kwamba kisa hicho kiliathiri wasichana karibu watano waliokuwa wakitaka kuabiri ndege uwanja wa ndege wa Denver.
Alisema wakala mmoja wa United alijaribu kuwashurutisha wasichana hao, mmoja wa umri wa miaka 10, kubadilisha mavazi yao na kuvalia marinda badala ya long'i hizo za kubana.
Alisema wasichana watatu kati ya hao waliruhusiwa kuabiri ndege baada ya kukubali kuvalia marinda, lakini hao wengine wawili walizuiwa kuabiri ndege.








Tweet from Shannon Watts reads: 1) 3 girls inspected for wearing perfectly acceptable leggings. 2 not allowed to board. I don't care what kind of passengers they were.

Haki miliki ya pichaTWITTER




Alishutumu shirika hilo, na kuuliza: "Ni wakati gani United waligeuka na kuwa polisi wa kuamua kuhusu mavazi?"


United baadaye walijibu kwenye Twitter wakisema wenye hati hizo maalum hutakiwa kufuata kanuni maalum za mavazi.



MGOGORO MZITO UNARIPOTIWA NDANI YA CHADEMA

Chama chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kimeingia katika wingu zito na kutishia kukisambaratisha chama hicho.

Chanzo cha Mgogoro ni nafasi za Ubunge wa Africa mashariki, Uchaguzi wa kanda ya Mashariki na Hali ya kifedha ndani ya chama.

Chanzo cha ndani ya CHADEMA kinasema kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe aliingia na majina mawili ndo akawaambia wayachague ambapo aliingia na Majina hayo ni Masha na Wenje hakukua na utaratibu sahihi wa kuwapata wagombea katika Bunge la Africa Mashariki.

Uchaguzi wa kumpata Viongozi ndani ya kanda ya Mashariki ulijaa kasoro nyingi ambapo wananchama wanaulinganisha na ule wa kanda ya Nyasa ambapo Ole Sosopi alitupwa nje ya kinyang'anyiro kwa kuwa mwenyekiti wa chama aliingia na Jina lake.

Idara ya fedha ndani ya CHADEMA haijakaa vizuri hivyo kuleta sintofahamu kwa wadhamini ambao wanataka ukaguzi wa fedha kupitia mkaguzi huru akague ili wajiridhishe wadhamini ndani ya CHADEMA wamekua wagumu kutoa fedha zao Hali ambayo inaisababishia chama ukata kwani Tajiri na Mdhamini mkubwa ndani ya CHADEMA ndugu Sabodo Alishajitoa na Kuungana na Rais Magufuli baada ya kuona Utendaji wake uliotukuka.