Tuesday, 28 March 2017

Remi: "Carlos the Jackal" afungwe maisha

Mwendesha mashitaka nchini Ufaransa Remi Crosson du Cormier ametaka Ilich Ramirez Sanchez anayejulikana kwa jina maarufu la Carlos the Jackal ahukumiwe kifungo cha maisha jela kwa shambulizi la guruneti 1974 mjini Paris lililowazua watu wawili. 

Kesi hiyo inatarajiwa kukamilika leo na hukumu kutolewa ingawa majaji watachukua muda zaidi kuizingatai hukumu hiyo. Wakili wa Carlos,
 Isabelle Coutant Peyre amesema kesi dhidi ya raia huyo wa Venezuela mwenye umri wa miaka 67 ni ya kisiasa. 

Carlos anatumikia vifungo viwili vya maisha kwa kuhusika na mashambulizi ya mabomu yaliyowaua watu 11 kati ya 1982-83 na kwa mauaji ya mawakili wawili wa polisi ya Ufaransa na afisa wa ujasusi wa Lebanon 1975.

Share this

0 Comment to "Remi: "Carlos the Jackal" afungwe maisha"

Post a Comment