Wakfu wake umesema amekufa katika hospitali moja mjini Johannesburg baada ya kuugua kwa muda mfupi kufuatia matibabu ya kupasuliwa ubongo.
Kathrada ni miongoni mwa watu walioshitakiwa katika kesi ya Rivonia 1964 iliyoibua hamasa kubwa kimataifa kuhusu ukatili wa utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kathrada alitumikia kifungo cha miaka 26 na miezi mitatu jela, 18 akiwa katika gereza maarufu la kisiwa cha Robben katika pwani ya mji wa Cape Town pamoja na rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.
Askofu mkuu wa Afrika Kusini aliyestaafu Desmond Tutu amemueleza Kathrada kuwa mtu aliyekuwa na wema na unyenyekevu na kumpongeza kama kiongozi aliyekuwa na maadili katika vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
0 Comment to "Mwanaharakati wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini afariki"
Post a Comment