Tuesday, 28 March 2017

Amnesty: Mashambulizi ya Mosul ni kinyume na sheria

     Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema mamia ya raia wameuawa katika mji wa Mosul nchini Iraq katika miezi ya hivi karibuni baada ya maafisa kuwaamuru wabakie majumbani mwao licha ya mashambulizi ya kutokea angani ya muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu mjini humo.

 Raia hadi 150 waliuliwa katika shambulizi la kutokea angani Machi 17 katika kitongoji cha al-Jadida mjini Mosul.

Shirika hilo limesema agizo la maafisa wa Iraq lina maana vikosi vya muungano vilitakiwa kufahamu idadi kubwa ya raia wangekuwa wahanga wa mashambulizi yoyote ya kutokea angani. 

Shirika la Amnesty International linasema kushindwa kuyazuia mashambulizi hayo huenda kumevunja sheria za kimataifa. Maafisa wa Marekani na Iraq wanachunguza shambulizi hilo pamoja na mengine.


Share this

0 Comment to "Amnesty: Mashambulizi ya Mosul ni kinyume na sheria"

Post a Comment