Monday, 27 March 2017

Waziri aagiza Nay wa Mitego aachiliwe huru Tanzania

Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe ameagiza msanii aliyekamatwa kuhusiana na wimbo wake alioutoa hivi karibuni aachiliwe huru. Sehemu ya maudhui ya wimbo huo inagusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania Mwanamuziki Ney wa Mitego akamatwa Tanzania Magufuli ayaonya magazeti Tanzania Nay wa Mitego hata hivyo ametakiwa auboreshe zaidi wimbo wake, kwa mujibu wa ujumbe uliopakiwa katika ukurasa Rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kwenye Twitter.
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali. Mapema leo, Baraza la Sanaa la Taifa Tanzania (Basata), lilikuwa limetangaza kuufungia wimbo huo kwa jina Wapo usichezwe kwenye vyombo vya habari au kutumika kwa namna yoyote ile. "Basata linawakumbusha wasanii na wadau wote wa kazi za sanaa kuzingatia ubunifu wa hali ya juu kufanya kazi za sanaa, hata kufikisha ujumbe mbalimbali wa kufundisha, kuelimisha, kuburudisha na hata kuonya," taarifa kutoka kwa baraza hilo ilisema. "Baraza linawaonya wale wote wanaotumia kazi zilizopigwa marufuku, ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi (na) hatua kali zitachukuliwa juu yao."

Share this

0 Comment to "Waziri aagiza Nay wa Mitego aachiliwe huru Tanzania"

Post a Comment