Sunday, 26 March 2017

JWTZ yatangaza kulipa Deni la Tanesco

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amethibitisha kuwa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) linadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni Tatu na Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco).
Jenerali Mabeyo amethibitisha hayo mapema leo wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na hatua walizochukua kufuatia kupokea barua ya Tanesco ambayo iliwataka walipe deni hilo mpaka kufikia kesho tarehe 27 Machi 2017 vinginevyo jeshi hilo litakatiwa huduma hiyo katika vikosi vyake vyote.
Aidha Jenerali Mabeyo amesema kuwa amewaagiza watendaji wake kufikia kesho Machi 27, 2017 wawe wamefikisha hundi (cheque) ya shilingi bilioni moja kwa Tanesco kuepuka kukatiwa huduma hiyo.

Share this

0 Comment to "JWTZ yatangaza kulipa Deni la Tanesco"

Post a Comment